Wafanyakazi serikalini miongoni mwa wadaiwa Sh bilioni 7 kodi ya pango

Wafanyakazi wa taasisi za Serikali ni miongoni mwa wapangaji wanaodaiwa kiasi cha Sh bilioni 7.8 kodi ya pango.

Kwa mujibu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wamesema baadhi ya watumishi wanaoishi kwenye nyumba hizo wanaodaiwa Sh bilioni 3.5.

“Kwa kipindi kirefu kumekuwa na ulimbikizaji wa madeni, umekuwa ukifanywa na watumishi wa imma lakini pia viongozi wa serikali, sasa jambo hili tumeliona na ni jambo ambalo linarudisha nyumba maendeleo ambayo wakala wa Majengo unatarajia kufanya” amesema Mtendaji Mkuu wa TBA Daudi Kondoro

Aidha TBA inaendelea na hatua za ukisanyaji wa madeni hayo kupitia njia ya mfumo maalum wa GRMS pamoja na kutumia wakala wa mahakama atakae zunguka Nchi nzima kufatilia na kuhakikisha madeni hayo yanalipwa.

Hata hivyo kwasasa miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi unaendelea kwa jiji la Dar es salaam na Arusha.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button