Wafukua kaburi, wanyofoa titi, moyo, jicho na ulimi

JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya linawatafuta watu waliofukua kaburi na kuchukua viungo vya marehemu likiwemo titi, moyo, jicho na ulimi. 

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Benjamin Kuzaga amesema kuwa Novemba 05, mwaka huu mkazi wa Kijiji cha Kilasi wilayani Rungwe, Neema Mlomba (26) alifariki dunia muda mfupi baada ya kujifungua mtoto wa kiume katika Hospitali ya Wazazi –Meta jijini Mbeya. 

Kamanda Kuzaga amesema Neema alizikwa katika makaburi ya Kamasulu–Mpunguti Kijiji cha Kilasi Halmashauri ya Busokelo, hata hivyo amesema asubuhi ya Novemba 07 mwaka huu, ndugu wa marehemu waligundua kuwa kaburi la Neema limefukuliwa na uchunguzi ulionesha kuwa viungo vya marehemu vilikuwa vimechukuliwa likiwamo titi la kulia, jicho la kulia, tumbo lilichanwa katikati, ulimi ulikatwa na moyo ulinyofolewa. 

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema matukio ya imani za kishirikina yakiwamo ya kujinyonga yamekuwa yakijitokeza mkoani humo na akatoa mwito kwa wakazi wa Mbeya waachane na vitendo hivyo.

Wakati huo huo, Jeshi la Polisi mkoani humo limethibitisha kutokea ajali iliyosababisha vifo vya watu wawili na wengine watatu kujeruhiwa. Kamanda Kuzaga alisema basi la kampuni ya Mangare Express liligongana na magari mengine mawili katika mteremko wa Iwambi-Mbalizi. 

Alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa gari ya Mangare Express uliosababisha ligonge gari dogo aina ya Toyota Raumu na kusababisha vifo vya watu wawili waliokuwa kwenye gari hiyo.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Brayson kaduma
Brayson kaduma
1 year ago

Haya mambo ya ushirikina ,ya pingwe kabisa ,maana yanaongeza hofu kwa wananchi, hebu tuwe na hofu ya mungu,lakini tunatakiwa kufichua maovu yanayojitokeza kama haya ,yanaharibu sofa ya taifa letu.

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x