Wafungwa 44 kufanya mtihani wa darasa la nne

MOROGORO:  VIJANA 44 ambao ni wafungwa katika Gereza la Wami Vijana mkoani Morogoro wanatarajiwa kufanya mtihani wa Taifa wa darasa la nne mwaka huu (2024) wakiwa wanaendelea kutumikia vifungo vyao Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Mzee Ramadhan Nyamka amesema.

Kamishna Jenerali Nyamka amesema katika ziara fupi ya Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) nchini, Shigeki Komatsubara, baada ya kutembelea baadhi ya magereza ya mkoa wa Pwani na Morogoro.

Nyamka amesema Mwakilishi wa Shirika hilo nchini alifanya ziara hiyo ikiwa ni kutimiza ahadi yake aliyoitoa Januari 30, mwaka huu wakati wa kusaini makubaliano ya ushirikiano kati ya UNDP na Jeshi la Magereza nchini.

Advertisement

Amesema moja na maeneo ambayo mwakilishi hiyo aliweza kuona shughuli zinafanywa na Jeshi hilo kwa lengo kuu la urekebishaji wa wafungwa nchini ni kwenye gereza la Wami Vijana ambalo lina wafungwa vijana wa miaka 18 hadi 25.

Amesema kuwa gereza hilo ni kama la wazi kwa ajili ya kutoa elimu na mafunzo ya stadi za kazi kwa wafungwa vijana.