‘Wafungwa mrudieni Mungu’

DAR ES SALAAM: WAFUNGWA na Mahabusu wa Gereza la Segerea mkoani Dar es Salaam wametakiwa kumuomba Mungu kwa unyenyekevu ili awaepushe na dhahama ama adha wanazopitia na kuwataka kubadirika kitabia baada ya kutumikia vifungo vyao.

Ushauri na mawaidha hayo umetolewa na Katibu wa Kanisa Halisi la Mungu Baba, Utawala Halisi lenye makao yake makuu Namanga-Tegeta mkoani Dar es Salaam walipotembelea gereza hilo kwa lengo la kuwaombea na kuwapatia zawadi mbalimbali kwa ajili ya kujikimu.

“Hupo hapa kwa bahati mbaya bali ni kwa kusudi na kwakusudi la aliyetuumba kuamua kukupitisheni katika hili basi muaminini Chanzo Halisi mwenyewe na kumuomba kwa unyenyekevu naye atawatendea wepesi na mtatoka mkiwa salama” amesema

Katibu huyo amewaeleza wafungwa na mahabusu kwamba Kainisa Halisi la Mungu Baba husimamia mambo matatu ambayo ni Amani, Upendo usiyobagua na Ibada ni uzalishaji na hivyo kuwasihi wafungwa hao baada ya kutumikia vifungo vyao wakatekeleze hayo ili maisha yao yawe mazuri na kumtukuza Muumba wa vyote.

“Kwahiyo ujio wetu hapa ni sehemu ya nguzo zetu za ibada hivyo hatunabudi kuwasihi kuishi Maisha yakumpendeza Muumba na kwakufanya hivyo hata siku za kukaa gerezani zitaisha kiurahisi na ikiwezekana hata kupata msamaha kwakuwa Muumba wa vyote hashindwi chochote akitolea mfano wa Paulo na sila walipopaza sauti kwa muumba naye aliwajibu na milango ya gereza ikafunguka”amesema

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha wafungwa na Mahabusu wa kike, ASP Hamida Matimba amelishukuru Kanisa hilo kwa mchango wa hali na mali kwa wafungwa wa gereza na hivyo kwaomba wasichoke kuwatembelea.

“Tumefarijika na ujio wenu msituchoke muendelee kututembelea na kutuombea kwakuwa binadamu hukumbwa na changamoto mbalimbali lakini kwa maombi changamoto zote huisha”

Habari Zifananazo

Back to top button