Waganga matapeli waonywa

MWANZA: Waganga wasio na mafunzo wala kusajiliwa wamepewa onyo na kutakiwa kuacha mara moja kwani kufanya hivyo ni kuvunja taratibu zilizowekwa.

Akizungumza katika hafla fupi ya kuwakabidhi vyeti wataalam wa tiba asili na tiba mbadala mara baada ya kuhitimu mafunzo ya siku saba yaliyoandaliwa na chuo cha Mwanza Polytechnic Institute

Katibu Tawala Msaidizi Miundombinu na Ubunifu Mkoa wa Mwanza Chagu Nghoma amesema kuwa kwa muda sasa wameibukua baadhi ya watu wanaojitangaza kuwa wao ni waganga wa tiba asili na tiba mbadala ilihali hawana usajili wowote wala hawatambuliki na mamlaka za Serikali na kusisitiza kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.

Advertisement

“Suala la matibabu sio la kuchezea kwani ni suala nyeti sana Serikali haitawavumilia waganga wa tiba asilia ambao ni matapeli kama lambalamba, kamchape ambao wanafanya biashara kwa kutumia mgongo wa tiba asilia”amesema

Aidha katika hatua nyingine Chagu amesema kuwa huduma ya tiba asili zimekua zikitumika kwa miaka mingi hapa nchini tangu enzi za mababu lakini kwa kutambua unyeti wa huduma hizo serikali iliona ni vyema ziboreshwe ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa wataalam hao.

“Haiwezekani ukatoa huduma kwa mgonjwa bila kujua anaumwa nini lazima upate vipimo vyake kwanza ili ujue kiini cha tatizo la mgonjwa ndipo uanze kumtibu”…. Amesisitiza

Awali akitoa taarifa kwa mgeni rasmi juu ya malengo ya mafunzo hayo mratibu wa mafunzo Dk.Sally Giyunga amesema kuwa wataalam hao wamefundisha mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuandaa dawa mbadala ,sheria ya tiba asili na mbadala ,ukusanyaji wa dawa ghafi na namna ya kuzikausha kupitia nishati ya jua namna ya kujikinga na kumkinga mteja  na magonjwa yakuambukiza na yasiyo ya kuambukizwa.

Abuu Jadawi na Milembe Kisinda ni wataalam wa tiba asili na tiba mbadala ambao kwa pamoja wamehitimu mafunzo hayo wameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kuwapa mwongozo mzuri wa kupata mafunzo ambapo wamesema kuwa mafunzo hayo yatawaongezea ufanisi wa utendaji kazi katika shughuli zao.

 

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *