Wageni 1,223 wazuiwa kuingia nchini

DODOMA;SERIKALI imesema imefanikiwa kuwazuia kuingia nchini kwa sababu mbalimbali jumla ya wageni 1,223 kwa kipindi cha kuanzia Januari 2022 hadi Mei 2024.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kigoma Mjini, Kilumbe Ng’enda aliyehoji mpango wa serikali kudhibiti wahamiaji haramu mipakani kabla hawaingia nchini.

“Serikali inaendelea kusimika mfumo wa kielektroniki wa mipaka (e – border), ambao unasaidia katika kudhibiti wageni wasio na sifa kabla hawajaingia nchini.

Advertisement

“Kwa kutumia mfumo huo Serikali imefanikiwa kuwazuia kuingia nchini kwa sababu mbalimbali jumla ya wageni 1,223 kwa kipindi cha kuanzia Januari 2022 hadi Mei 2024.

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kufanya vikao vya kikanda, kimataifa na ujirani mwema kwa lengo la kupanga mipango ya pamoja ya kudhibiti uhamiaji haramu,” amesema Waziri Masauni.