Wageni CAF kuishuhudia Yanga Mkapa

AFISA Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema timu hiyo inatarajiwa kupokea wageni zaidi ya 200 kutoka Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kwa ajili ya mchezo wao fainali dhidi ya USM Algers.

Kamwe anasema kutokana na ugeni huo mkubwa wanafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha wanakamilisha taratibu zote kuelekea mchezo huo mkubwa Afrika hivyo watanzania waondoke shaka kwenye hilo.

Katika hatua nyingine Afisa habari huyo anasema baada ya kuona muelekeo mzuri kuelekea mchezo huo siku ya kesho ijumaa wataandaa tukio kubwa lililopewa jina la shangwe la CAF litakatofanyika Zakhiem Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.

Advertisement

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *