PWANI: KLABU ya Rotary ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Taasisi ya African Youth Foundation imepanda miche ya miti 1,000 kwenye Msitu wa Hifadhi ya Kazimzumbwi iliyopo Mkoa wa Pwani ikiwa ni sehemu yake ya mkakati wa kuhifadhi mazingira .
Hayo yamesemwa Machi 23 ,2024 na Rais wa klabu hiyo, Nikki Aggarwal wakati wa upandaji wa miche hiyo.
Ameongezea kwa kusema kuwa wamepanda miti hiyo kutokana na kuwa na mradi wao wakutoa madawati kwa shule za umma hapa nchini kwani madawati hayo yanatumia mbao.
Wanachama wa Rotary Klabu Manisha Tanna na Nirmal Sheth wamesema upandaji wa miti hiyo unawapatia wananchi hewa safi pamoja uhifadhi mzuri wa mazingira.
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji kutoka Taasisi ya Africa Asia Youth Foundation amesema wamepanda miti hiyo kwa kushirikiana na vijana 100 kwani misitu hiyo inachangia hewa ya Oxygeni kwa asilimia 80% kwa Mkoa wa Dar es salaam.
Ikumbukwe hii ni wiki ya misitu hivyo upandaji wa miti hiyo unaendana sambamba na wiki hiyo.