Wahamiaji haramu 65 wakamatwa Katavi

WAHAMIAJI haramu 65 kutoka nchini Ethiopia wamekamatwa katika Wilaya ya Mlele mkoani Katavi wakiwa katika gari la kubebea mafuta wakisafirishwa kutoka Mwanza kuelekea nchini Zambia.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Majid Mwanga amesema raia hao wa kigeni waliokua wakisafirishwa bila kufuata utaratibu wamekamatwa katika kijiji cha Kamsisi wilaya hiyo wakiwa wamebebwa katika gari la kubebea mafuta .

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mlele, Soud Mbogo amesikitishwa na baadhi ya madereva kukiuka taratibu za matumizi ya vyombo vya usafirishaji.

Advertisement

Dereva wa lori hilo la mafuta, Msadick Msomolo amedai kuwa alipewa kazi hiyo na kaka yake aliyemfundisha kazi ya udereva na kumuahidi pesa nzuri endapo watafanikisha mpango huo.

Hata hivyo raia hao kwa sasa wamekabidhiwa kwa Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Katavi kwa ajili ya taratibu zingine za kisheria.

6 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *