Wahamiaji haramu wakamatwa shamba la michungwa

RAIA tisa wa Ethiopia na Mtanzania wamekamatwa wilayani Handeni mkoani Tanga wakiwa wamefichwa kwenye shamba la michungwa.

Kaimu Ofisa Uhamiaji Wilaya ya Handeni, Mkumbo Gideon alisema jana kuwa walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kuna watu wamefichwa kwenye shamba hilo.

Gideon alisema walifika eneo ambalo walionekana wahamiaji haramu hao katika Kijiji cha Ngojolo Kata ya Kwamgwe wakakuta wamefichwa wakisubiri usafiri kwa ajili ya kuendelea na safari.

Alisema raia hao tisa walikuwa na mwenyeji wao Mtanzania mkazi wa Hale, Hassan Ramadhani anayetuhumiwa kuratibu usafiri wa kuwasafirisha kwenda sehemu nyingine.

Habari Zifananazo

Back to top button