“Wahandisi waendane na teknolojia”

WAHANDISI wametakiwa kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake kuwa wabunifu na wenye uwezo wa kuendana na mabadiliko ya haraka ya teknolojia.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa TANROAD, Mhandisi Mohamed Besta kwenye maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Duniani leo Machi 4, 2024 jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo wenye lengo la kukuza ubunifu na kuleta maendeleo endelevu katika nchi wenye Kauli mbiu ya “Suluhu za Wahandisi katika Ulimwengu Endelevu”, ikisisitiza umuhimu wa ubunifu katika kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia na kuleta maendeleo endelevu.

Kwa upande wake Rais wa Taasisi ya Wahandisi Tanzania, Dk Gemma Modu amesisitiza umuhimu wa wahandisi kujitahidi kuwa wachangiaji hai katika maendeleo endelevu na sio watazamaji pembeni katika jitihada ya kutumiza azma hiyo amewaalika wanafunzi wa sekta ya uhandisi kujifunza kutoka kwa wataalamu na kujiandaa kikamilifu kwa changamoto za siku zijazo.

Naye Chedi Masambaji, Rais wa Waandisi Washauri, amesisitiza umuhimu wa kuwa wabunifu na kutumia teknolojia katika kuleta maboresho katika sekta mbalimbali kama miundombinu na usafirishaji.

Habari Zifananazo

Back to top button