Wahandisi washauri kuongezewa ujuzi

BODI ya Usajili wa Wahandisi (ERB) imetakiwa kuongeza wigo kwa kuwapa uwezo wahandishi washauri kuhakikisha ujuzi unakuzwa katika miradi mbalimbali kwa maendeleo ya taifa.

Akizungumza leo Februari 8, 2024 katika mkutano uliomkutanisha Mwenyekiti na Wajumbe wa ERB, Bashungwa amesisitiza kuweka mikakati ya uendelezaji wa wahandisi washauri kukuza sekta hiyo.

“Vipaumbele na maagizo ya Mheshimiwa Dk Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika sekta hii ni kuona ushiriki mkubwa wa Wahandisi na Makandarasi Wazawa katika kazi za ujenzi na usimamizi wa miradi (Local Content), sisi kama wasaidizi wake tuhakikishe tunalitekeleza hili”.amesema Bashungwa.

Aidha, ameelekeza ushirikishwaji wa wahandisi wahitimu katika mpango wa mafunzo kwa vitendo (SEAP) kwenye miradi mikubwa inayotekelezwa nchini ili kuwajengea uwezo

Habari Zifananazo

Back to top button