Wahandisi watakiwa kuchangamkia fursa za miradi

SERIKALI imeahidi kuendeleza, kuibua, kutambua, kukuza na kuendeleza ubunifu unaofanywa na wahandisi wazawa kwa maendeleo endelevu ya Taifa.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema hayo wakati akifungua maadhimisho ya 19 ya siku ya wahandisi nchini, ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza umuhimu wa kuzingatia sheria ya kuwawezesha wazawa katika ujenzi wa miradi, ili kunufaika kiutalaamu, kiuzoefu na kiuchumi.

“Wahandisi ndio nguzo muwe na weledi na umakini katika kusimamia miradi, ili iwe bora yenye gharama nafuu na inayokamilika kwa muda uliopangwa,” amesisitiza Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa ameaigiza Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), kuchukua hatua stahiki za kisheria na za haraka kwa kampuni ya kihandisi, taasisi na wahandisi wasio waadilifu.

Amesema serikali itaendelea kutekeleza miradi mingi ya kimkakati katika kujenga miundombinu na uchumi wa nchi, hivyo ni jukumu la wahandisi kuitumia fursa hii muhimu kujenga Taifa lao.

 

Habari Zifananazo

Back to top button