Wahimizwa ubora wa mazao soko la nje

MOROGORO: WAKULIMA wa Tarafa ya Mgeta ,Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro wameiomba Serikali pamoja na Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) kukaa meza moja na kutatua changamoto zilizopo kwenye soko la Nyandira ili kulifanya kuwa endelevu katika kuwezesha ukuaji wa uchumi.

Wakulima hao waliwasilisha ombi hilo kwa serikali ya wilaya na mkoa wakati walipotoa shukrani zao kwa Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Anne Sophie Ave ambaye alitembelea soko la Nyandira ambalo Serikali ya nchi yake ilitoa ufadhili wa fedha za ujenzi.

Mkulima wa kikundi cha Bega kwa Bega na Mwanamtandao waa Kata ya Tchezema, Otensia Thomas amesema Soko hilo limejengwa na MVIWATA kwa ufadhili wa Serikali ya Ufaransa baada ya wazo ambalo liliubuliwa wakulima mwaka 2002 na mradi wa ujenzi kukamilika mwaka 2004.

Amesema baada ya kukamilika ujenzi wake ,wakulima walikuwa wanasimamia wenyewe soko hilo kwa makubaliano mbalimbali kati ya serikali, halmashauri na Mviwata.

“Soko hili kimsingi linasaidia wakulima wa tarafa ya Mgeta na wilaya ya Mvomero , na wakilima wameweza kuinua hali zao za maisha, wamejenga nyumba bora , kupeleka watoto shule na watu wengine wameweza kujiajiri katika shughuli mbalimbali za kilimo, ushonaji na mama lishe eneo la soko,”amesema Otensia.

Pamoja na hayo amesema kuanzia mwaka 2016, Soko la Nyandira lipo chini ya Serikali katika usimamizi wake huku Mviwata wapo kwa ajili ya kuangalia vikundi vya wakulima vinanufaika na soko, hivyo kwasasa linapaswa kuendelea kufanyiwa ukarabati wa mara kwa mara liwe endelevu.

Naye Mkulima na mkazi wa Nyandira , Bononasi Mwiache amesema kujengwa kwa soko hilo pamoja na barabara ya zege kumewaletea faraja na kuwaondolea adha ya kubeba mizigo na kwenda soko la Langali lililopo umbali wa kilometa 15 .

Mwiache amesema kabla ya kujengwa kwa soko hilo ,wakulima walikuwa wanatembea umbali huo wakibeba mizigo kichwani kufikisha katika soko lilolopo kwenye kijiji hicho kuyaunza kwa wanunuzi.

Akijibu changamoto za wakulima hao , Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Maulid Dotto ameahidi kuwa Serikali itazifayia kazi changamoto hizo na kuzitafutia ufumbuzi kwa haraka ili kuhakikisha maboresho ya mindombinu wezeshi ndani ya soko hilo yanafanyika ili waendelea kunufaika kwa kuuza mazao yao.

Kwa upande wake Balozi wa ufaransa nchini Anne Sophie Ave alifurahishwa kwa kuona wakulima wanalitumia vyema soko hilo ambapo aliwahimiza kuendelea kuongeza uzalishaji wa mazao kwa wingi na yenye viwango vya ubora kuwezesha yapate soko la nje ya nchi.

Balozi wa Ufaransa hapa nchini amesema, Tanzania na Ufaransa zinashirikiana katika sekta ya kilimo kwa miaka mingi na mfano katika soko wa Nyandira ambao ni mradi wa miaka 30 iliyopita na unaendelea kufanya kazi.

“Nimebahatika kukutana na wakulima wa Nyandira , tumeona mashamba ya milimani na uzalishaji wa mazao , nilipenda zaidi wakati wa chakula cha mchana kimeandaliwa cha asili ya Kitanzania,”amesema Balozi Anne.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button