“Wahitimu vyuo vikuu watatuzi changamoto za jamii”
WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema vyuo vikuu ni viwanda vya kupika wataalamu wa nyanja mbalimbali ambao baada ya masomo yao watatoka na tafiti zao kwenda kutatua changamoto za kijamii.
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Carolyne Nombo alisema hayo katika hotuba yake wakati utoaji wa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi kwenye masomo yao na kwa watafiti waliofanya vizuri kwenye tafiti zao.
Hafla ya utoaji zawaidi 248 kwa washindi ilifayika Chuo Kuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Kampasi kuu ya Edward Moringe , mkoani Morogoro.
Profesa Nombo amewataka watafiti, wahitimu na wahadhiri waliopo kwenye vyuo vikuu nchini watambue wanaowajibu wa kutatua changamoto mbalimbali kwenye jamii kupitia tafiti zao.
Katibu mkuu wa wizara hiyo amewataka watafiti nchini kuwa tafiti zao zitoke kuifikia jamii ili zitumike kutatua changamoto ambazo jamii inakabiliana nazo.
“Mtafiti endapo utafiti wake utabaki kwenye makaratasi hautakuwa na maana yoyote kama hautaifikia jamii kwa ajili ya kutatua changamoto zinazowakabili.
” amesema Profesa Nombo
“ Utafiti ambao umefanyika na hasa watafiti hawa waliobuka kidedea tunatarajia utafiti wao utoke na kwenda kutatua l changamoto mbalimbai zilizopo kwenye jamii …tunafahamu utafiti huwa unafanyika kutatua changamoto ya kijamii “ amesema Profesa Nombo
Katibu mkuu amesema utafiti inaoleta manufaa katika jamii unaonesha maana halisi ya Vyuo Vikuu kuwa ni viwanda vya kupika wataalamu wakutatua changamoto kwenye jamii .
“Mwanafunzi ambaye ana pata GPA kubwa , hiyo haitakuwa na maana kama hataweza kurudisha kwa jamii itachangia maendeleo na ukisoma bila kutatua tatizo lililipo kwenye jamii , elimu yako inakuwa haipo “ amesema Profesa Ndombo
Pia amewashauri wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu kutumia elimu na ujuzi walioopata kuzalisha ajira za kujiajiri kutokana na stadi za ujuzi waliupata wakiwa vyuoni.
Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, Profesa Raphael Chibunda amesema malengo makubwa ya kutoa hizo zawadi ni kuwafanya wanafunzi kuwa na ushindani kati yao .
Profesa Chibunda amesema ,kwa miaka mitano mfululizo idadi ya wanafunzi wakike wanaofanya vizuri na kupata zawadi imeongezeka ingawa chuo kina asilimia 42 ya wanafunzi wakike .
Makamu mkuu wa Chuo Kikuu hicho alisema , katika kuendeleza watafiti wachanga na wabunifu kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kimetenga Sh bilioni 1 .
Profesa Chibunda amesema, Chuo Kikuu hicho sawa na vyuo vikuu vingine, kimepitia na kuboresha mitaala yake ili kuwezesha kuwa na wahitimu wenye kuajirika na kujiajiri wenyewe baada ya kuhitimu masomo yao..