RC Arusha ataka uwekezaji zaidi huduma ya vyakula

MKUU wa Mkoa wa Arusha, John Mongela ametaka uwekezaji zaidi jijini jijini Arusha hasa katika masuala yanayohusu vyakula, ili kuongeza kasi ya uwepo wa vyakula vitakavyovutia watalii jijini humo.

Ametoa rai hiyo leo Februari 13, 2024 wakati wa uzinduzi wa mgahawa wa KFC na kuwataka kuongeza matawi zaidi mkoani hapo, ili kuwezesha  wananchi wanaotumia huduma za vyakula kuvipata kwa ukaribu.

RC Mongela amesema huduma bora ya chakula ni muhimu kutolewa Arusha, ili kuwavuta zaidi watalii na wananchi kwa ujumla kupata vyakula vya uhakika na kuomba KFC kufunga matawi mengine zaidi jijini humo.

Akizungumzia uamuzi wa kufungua KFC jijini hapa, Mkurugenzi Mtendaji wa Dough Works,Vikram Desai amesema hiyo ni hatua muhimu kwa Tanzania kuwafikishia wananchi huduma bora ya chakula, lakini pia inachangia ajira kwa Watanzania

 

Habari Zifananazo

Back to top button