Wahukumiwa jela maisha kwa ubakaji

WATU wawili wamehukumiwa kwenda jela maisha baada ya Mahakama ya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara kuwatia hatiani kwa kosa la ubakaji.

Akitoa taarifa hiyo leo kwa waandishi wa habari mkoani humo, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara ACP, Necodemus Katembo amesema watuhumiwa hao ni wakazi wa kijiji cha makulani wilayani humo ambapo walitenda tukio hilo kwa nyakati tofauti.

Amewataja kwa majina watuhumiwa hao kuwa ni Omari Salumu (70) ambapo Novemba 22, 2023 alihukumiwa kwenda jela maisha na Mahakama hiyo kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka sita.

Mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Novemba 17,2023 majira ya saa 5:00 asubuhi kijijini hapo ambapo alikamatwa na kufikishwa kituo cha polisi wilayani humo.

Mtuhumiwa mwingine ni Emmanuel Dastan (32) aliyehukumiwa kifungo hicho na Mahakamani hiyo Novemba 17,2023 kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka sita (mwanafunzi wa chekechea katika shule ya msingi mkulani) ambapo wote ni wakazi wa kijijini hapo.

Tukio hilo alitenda majira ya saa 9:30 alasiri ambapo mtuhumiwa alikamatwa na kufikishwa katika kituo cha polisi.

“Jeshi la polisi linatoa wito kwa wananchi wote mkoa wa Mtwara kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kukomesha kabisa matukio ya kihalifu hasa unyanysaji dhidi ya watoto”amesema Katembo

“Hatua kali na za kisheria zitaendelea kuchukuliwa ili kuhakikisha Mkoa unaendelea kuwa shwari bila vitendo vya uhalifu”

Habari Zifananazo

Back to top button