Wahukumiwa kifungo jela kwa kosa la kunajisi

MTU mmoja aliyetambulika kwa jina la Lazaro John (19) amefungwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kulawiti mwanafunzi wa darasa la saba na mwingine aliyetambuliwa kwa jina la Fredrick Mollole (22) amefungwa kifungo cha miaka 30 kwa kosa la kumbaka mwanafunzi sekondari katika matukio mawili tofauti yaliyotokea wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Mshitakiwa mwingine aliyetambuliwa kwa jina la Emmanuel Wilson (14) yeye kwa kuwa ni mtoto chini ya miaka 18 amefungwa kifungo cha miaka miwili jela na atapelekwa katika gereza la watoto mkoani Mbeya kwa kosa la kumlawiti mwanafunzi kwa kushirikiana na mshitakiwa John.

Akisoma hukumu katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru mkoani hapa, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mwamini Kazema alisema kuwa ametoa hukumu baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi wanne wa upande wa Jamhuri na vielelezo vilivyowasilishwa katika mahakama hiyo.

Hakimu Kazema alisema kuwa ushahidi wa mashahidi watatu wa upande wa utetezi haukumshawishi yeye kuwaachia huru washitakiwa kwa kuwa ushahidi wao haukuwa na nguvu kisheria kuachiwa huru.

Baada ya kutiwa hatiani mshitakiwa John alipewa nafasi ya kujitetea na aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwa kuwa kosa hilo ni mara yake ya kwanza na shetani alimpitia na kujikuta akitenda kosa hilo.

Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Grace Madikenya alimuomba hakimu kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa kwani vitendo vya kulawiti watoto wadogo wamekithiri wilayani Arumeru ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia hiyo chafu kwa jamii.

‘’John ninakufunga kifungo cha maisha jela kwa kukutwa na shitaka hilo baada ya mimi kulidhika pasipo shaka yoyote na ushahidi uliotolewa na umetenda kosa hilo kwa kudhamiria ili  iwe fundisho kwa wengine,’’

‘’Na mshitakiwa Wilson kwa kuwa wewe ni mtoto ninakufunga miaka miwili katika gereza la watoto watukutu katika gereza lililoko mkoani Mbeya ili uende ukafundishwe maadili mema kwa jamii na ukitoa uwe raia mwema kwa wengine’’ alisema Kazema

Tukio hilo lililotokea Aprill 15 mwaka huu ambao washitakiwa hao John na Wilson walitenda kosa eneo la Soko 2 wilayani Arumeru mkoani Arusha baada ya kumteka na kumbeba mwanafunzi wa kiume wa darasa la saba wa shule ya msingi Soko 2 (jina limehifadhiwa) na kwenda kumlawiti nyumbani kwa Wilson hadi Aprill 26 kabla ya kukamatwa siku hiyo.

Kwa Mujibu ya maelezo ya awali waliosomewa washitakiwa hao ilidaiwa kuwa baada taarifa kuzagaa za mwanafunzi huyo kutoonekana nyumbani kwa wazazi wake msako mkali ulifanyika sokoni 2 Arumeru na taarifa fiche zilipelekwa kwa balozi kuwa mwanafunzi yuko katika chumba anachoishi Wilson.

Maelezo hayo yaliendelea kusema kuwa na askari, balozi na raia wengine walipokwenda nyumba hiyo walimkuta mwanafunzi huyo ndani akiwa na washitakiwa hao wawili huku akiwa ameshaharibiwa vibaya kwa kulawitiwa kwa pamoja na washitakiwa hao.

Washitakiwa hao walikamatwa siku hiyo na kufunguliwa shitaka la kulawiti mei 30 mwaka huu katika kituo chya polisi Arumeru na kesi ilianza kusikilizwa mwezi juu na hukumu hiyo kutolewa na hakimu Kazema leo.

Naye Mshitakiwa Fredrick Mollel, 22, amefungwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa kidatu cha pili wa miaka 15 wa shule ya sekondari ya Enyoito iliyopo Sokoni 2 wilayani Arumeru Arusha.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi wilayani Arumeru  , Mwamini Kazema alisema kuwa ametoa adhabu hiyo baada ya kuridhishwa na ushahidi ulitolewa mahakamani hapo na kusema kuwa utetezi wa washitakiwa haukuwa na nguvu ya kuwaachia huru washitakiwa hao

Mollel alipopewa nafasi ya kujitetea baada ya kutiwa hatiani aliomba kupunguziwa adhabu kwa kuwa kosa hilo ni mara yake ya kwanza na wazazi wake wanamtegemea.

Mwendesha mashitaka wa serikali, Grace Madikenya alimuomba hakimu kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa wengine kwani vitendo vya ubakaji vimekuwa vikishika kasi kwa sasa na hatari kwa jamii.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Zambia Revenue Authority
Zambia Revenue Authority
1 month ago

Zambia Revenue Authority

MAPINDUZII.PNG
julizaah
julizaah
Reply to  Zambia Revenue Authority
1 month ago

Are you tired with your job good opportunity be09 Online Working Home Base Jobs for you here.

Copy This Site…………………………………. http://www.join.salary49.com

Last edited 1 month ago by julizaah
Sharon Smith
Sharon Smith
Reply to  julizaah
1 month ago

I’ve profited $17,000 in just four weeks by working from home comfortably part-time. I was devastated when I lost my previous business right away, but happily, I found this project, which has allowed me to get thousands of dollars from the comfort cfs06 of my home. Each person may definitely complete this simple task and earn extra money online by
visiting the next article———>>> https://tradecash1.blogspot.com/

Last edited 1 month ago by Sharon Smith
John Pombe Joseph Magufuli
John Pombe Joseph Magufuli
1 month ago

Zambia Revenue Authority

MAPINDUZI.jpg
Back to top button
4
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x