Waiomba serikali kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji

UMOJA wa wakulima wamwagiliaji walio chini ya mwamvuliwa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) kutoka l kijiji cha Mkoka wilayani Kongwa mkoani Dodoma, wameiomba Serikali iwaimarishie miundombinu ya umwagiliaji katika kilimo cha Alizeti Mkoka.

“Suluhisho pekee ni kutujengea kisima cha uhakika jamboambalo litatua migogoro ya mara kwa mara baina ya wakulimana wafugaji kwani imejengeka dhana ya kuwa, wakulimahutumia maji mengi katika shughuli za umwagiliaji katika eneo hilo,”

“Imefikia hatua ya kupelekwa katika Serikali ya Kijiji kujibutuhuma za matumizi mabaya ya maji katika umwagiliaji nakutulazimu kusubiri kwa siku kumi katika kupeana zamu zamatumizi ya maji jambo ambalo udhoofisa mimea yetu yenyeuhitaji wa maji katika ukuaji wake.”

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa kikundi cha umoja wamwagiliaji wa mazao waliopo katika kijiji cha Mkoka wilayaniKongwa mkoani Dodoma, Rajabu Singo wakati wa mahojianovmaalum na waandishi wa habari waliotembelea kujionea shambadarasa la mbegu za alizeti juzi.

Tumekuwa na migogoro ya mara kwa mara na wafugajikugombania maji yatokanayo na mto unapita karibu na shambaletu na kuwekewa ratiba maalumu ya umwagiliaji mazao yetukila baada ya siku 10 jamabo ambalo huathiri ukuaji wa mimeainayo hitaji maji katika ukuaji wake, “Singo alisema 

Taasisi ya kuboresha mifumo ya masoko ya kilimo nchini (AMDT) wakishirikiana na Taasisi ya Maendeleo ya Kilimo Denmark Asia (ADDA) imekuwa mstari wa mbele katikakuwaelimisha wakulima katika matumizi mbegu bora nateknolojia ya kilimo cha kisasa katika kuleta tija ya mazao yanayozalishwa.

Ozniel Benego ambaye ndiye kpatibu wa umoja wa wana kikundicha umwagiliaji, alisema, “jumla ya wanakikundi 35 tulipatiwamafunzo ya namna ya uzalishaji bora wa mazao kupitia Taasisiza AMDT na ADDA” kati ya hao wanachama 14 wamekuwamfano wa kuigwa baada ya kulima mbegu za alizeti katikashamba darasa lenye ukubwa wa hekari 25.

Kusema ukweli elimu tuliyopatiwa, imeongeza tija katikauzalishaji wa zao la alizeti na mahindi kwani, miongoni mwa mafunzo tuliyo patiwa ni pamoja na upimaji wa afya ya udongo kinachoambana na kilimo hai kinachotumia mbolea za asili.

Kwa upande wake, Victoria Mwerya ambaye ni mkulima wakijiji hicho alisema, “awali tulikuwa tumezoea kilimo cha msetokwa kuzika mbegu za mazaolakini kwa sasa tumejifunza kupanda mbegu bora kwa kutumia vipimo stahiki jambo ambalohulea tija katika mazao ya chakula na biashara.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Www.BizWork1.Com
1 month ago

Making additional money each month by performing a simple online task. Just by dedicating two hours a day to my home-based profession, I was able to earn and get $18,539 last month. Simple enough that even a youngster may learn how to do it and begin earning money online.
.
.
Detail Here———————————————————————–>>>  http://Www.BizWork1.Com

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x