Waiomba serikali kuwaondoa waharibifu miundombinu ya maji

BAADHI ya Wananchi wa kata ya Chanika wilayani Karagwe mkoani Kagera wameiomba serikali kuwaondoa watu waliovamia vyanzo vya maji na kuanzisha shughuli za kibinadamu hali inayochangia kukauka kwa vyanzo vyake.

Wananchi hao walisema hatua hiyo itasaidia kufanya miradi hiyo ambayo imetumia gharama kubwa ya  fedha za serikali kuwa endelevu huku wakitaka elimu juu ya athari ya uvamizi wa vyanzo hivyo kutolewa mara kwa mara.

Advertisement

Murshid Abudul mkazi wa Chanika alisema kuwa endapo hatua za haraka hazitachukuliwa kwa kuwaondoa Wananchi wanaofanya shughuli za ujenzi kilimo na mifugo huenda adha ya maji Karagwe   ikarudi baada ya miaka michache ijayo.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyeambatana na Kamati ya Siasa Wilaya ya Karagwe na Kamati ya Ulinzi na Usalama kukagua mradi wa maji Chanika, Paschale Rwamugata alikemea wananchi ambao wanajaribu kuendelea na shughuli zao  kuharibu  vyanzo vya maji huku akiwataka kusogea mbali kama sheria na sera za maji zinavyotaka.

“Naomba kuwahoji Wananchi wachanika serikali ikisema wananchi wa kata hii mchangie maji Sh bilioni 1 mtaweza kulala ,kama hamuwezi ni kwa nini hamutaki kuacha kuchezea vyanzo vya maji ??naomba mlinde vyanzo vya maji kama mboni yenu,Chama Cha Mapinduzi hakitamvumilia mtu anayeharibu vyanzo vya maji  hivyo naomba msitishe shughuli zenu mara moja katika vyanzo vya maji. “alisema Rwamugata

Katika ukaguzi wa mradi huo alilidhishwa na namna Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) inavyopambana kusimamia miradi ya maji na kuwakomboa Wananchi katika adha kubwa ya kufata maji umbali mrefu  na kuendelea na shughuli za kiuchumi huku akikiri kuwa miaka mingi iliyopita Wilaya ya Karagwe iliteseka na maji  mpaka baadhi ya watumishi waliogopa kufanya kazi za umma katika wilaya hiyo kutokana na changamoto ya hiyo.

/* */