Waishukuru Korea Kusini kusaidia huduma za afya

NAIBU Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Dk Julieth Magandi amesema Serikali ya Korea Kusini kupitia vyuo na taasisi zake, imekuwa na ushirikiano uliowezesha hospitali kuongeza ufanisi katika utoaji huduma bora kwa wananchi.

Dk Magandi amesema hayo leo alipokutana na madaktari, wakufunzi na wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Kosin na Yonsei vya nchini Korea Kusini, ambao wametembelea MNH Mloganzila kwa lengo la kujifunza na kujadiliana namna ya kuendelea kuboresha na kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya taasisi hizo.

Dk Magandi ameongeza kuwa kupitia ushirikiano huo, Taasisi ya Korea Foundation for Health Care imeweza kukarabati Wodi ya watoto wachanga chini ya siku 28 (NICU, ambapo ukarabati huo umewezesha wodi hiyo kulaza watoto 60 kwa wakati mmoja kutoka watoto 30 hapo awali.

“Pamoja na kukarabati sehemu hizi za kutolea huduma tumekuwa tukipata msaada wa vifaa tiba, pia wataalamu wetu wamepata fursa ya kujengewa uwezo ambapo mpaka sasa takribani watumishi 80 wamepata mafunzo ya muda mrefu na mfupi nchini Korea” amesema Dk Magandi.

Amebainisha kuwa Serikali ya Korea Kusini imekuwa ikileta wataalamu kwa lengo la kuwajengea uwezo wataalamu wa ndani, ambapo hivi karibuni MNH-Mloganzila kwa kushirikiana na daktari bingwa kutoka nchini humo, imefanikiwa kufanya upasuaji wa kupandikiza figo kwa wagonjwa watatu kwa mafanikio makubwa.

Kwa upande wake Mshauri wa Taaluma kutoka Chuo Kikuu cha Yonsei Prof. Sunjoo Kang, ameupongeza uongozi wa MNH-Mloganzila kwa namna inavyoendelea kuboresha huduma za afya, ndio maana kila mara wamekuwa wakivutiwa kuleta wanafunzi wao kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu.

Prof. Kang ameongeza kuwa vyuo hivyo vitaendelea kushirikiana na Mloganzila kwa kubadilishana ujuzi na uzoefu katika maeneo mbalimbali ya kibobezi kwa kuleta wataalamu wao katika hospitali hii na wataalamu wa MNH-Mloganzila kwenda katika vyuo hivyo kujifunza.

Naye Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Upasuaji Dk Godlove Mfuko amefafanua kuwa ziara hiyo imekuwa na manufaa, kwani madaktari, wakufunzi na wanafunzi hao wametembelea maeneo mbalimbali ya kutolea huduma, ambapo pia itawezesha kujadiliana namna wanavyoweza kuimarisha na kutanua wigo wa ushirikiano huo.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Annette M. Hamilton
Annette M. Hamilton
2 months ago

I’m remodeling $960 per day using my phone part-time. I’m presently on my fifth record for $27,000 and each one I’ve made has been from replicating and pasting photographs off the internet. This industry helps the United States generate more nd34 money every day for certain goals and tasks, and the quality earnings are just amazing. More information may be found
.
.
In this article————————————— >>> https://www.pay.hiring9.com.

Last edited 2 months ago by Annette M. Hamilton
Angela Cook
Angela Cook
Reply to  Annette M. Hamilton
2 months ago

I’ve earned $17,910 this month by working online from home. I work only six hours a day despite being a full-time college student. Everyone is capable of carrying out this work from their homes and learning it in spare time on a continuous basis.
To learn more, see this article———>>> https://workscoin1.pages.dev/

Last edited 2 months ago by Angela Cook
Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x