Waishukuru serikali mazingira rafiki taasisi za fedha

WAKALA ambaye anafanya huduma za kifedha Emmanuel Mnema, ameishukuru Serikali kwa kuandaa mazingira mazuri kwa taasisi za kifedha na kusababisha kuongezeka kwa ajira kwa vijana na kupunguza changamoto ya ajira.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam wakati akiwakilisha mawakala zaidi ya 200, wanaofanya kazi katika taasisi za benki mbalimbali ikiwemo benki ya I & M , Mnema alisema kwa zaidi ya mwaka mmoja amekuwa wakala wa bank na kujitengenezea kipato kikubwa na kuacha kuwa tegemezi.

Alisema katika huduma hizo anawaongeza sana benki ya I & M ambapo imeuwa miongoni mwainayotoa huduma kupitia mawakala wa mtaani, kwa kufanya kazi karibu na wateja wake na kufanya huduma hiyo kuwa rahisi kwakuwa huduma za kifedha kwa njia ya mashine za Kieletroniki imekuwa na changamoto nyingi.

Mkurugenzi wa benki hiyo,  Zahid Mustafa alisema taasisi hiyo imezisikia changamoto nyingi za wateja wake hasa ya ukosefu wa huduma ya huduma ya wakala, hivyo wamaamua kusajili rasmi mawakala zaidi ya 200 huku lengo likiwa kuwafikia mawakala 500 nchi nzima.

Alisema huduma ambayo itakuwa ikipatikana ni kutoa fedha kwa kiwango chochote kupitia wakala, huku wakiwa na uzoefu mkubwa katika huduma za kifedha kwa njia ya miaka mingi hasa kupitia kupitia mitandao ya kidigali ikiwemo Simu banking.

“Mawakala wataweza kupata kamishani mzuri tena kwa wakati kwakuwa lengo letu ni kuendelea kutoa huduma kwa wateja ili na wao wapate kujiajili” alisema.
Mustafa alisema huduma ambazo zinaweza kutolewa na bank hiyo kupitia mawakala watakaokuwa wakipatikana mtaani ni kuweka fedha, kutoa na kuangalia salio hii itapunguza watu kwenda katika ofisi za bank kwaajili ya kupata huduma.

Habari Zifananazo

Back to top button