SHEKHE Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Zubeir amewataka waislamu nchini pamoja na taasisi za dini kuwatumia wataalamu mbalimbali kwa ajili ya kuzifikia fursa za kimaendeleo zilizopo, ili kuhakikisha wanainuka kiuchumi.
Rai hiyo ameitoa leo wakati wa kongamano la maendeleo ya Waislamu nchini lililofanyika mkoani Tanga na kuesema ili waweze kuimarika kiuchumi, ni lazima wahakikishe wanawatumia wataalamu waliopo.
Amesema kwa miaka mingi taasisi za dini ya kiislamu pamoja na waumini wake wameshindwa kuwatumia wataalamu wa fani mbalimbali , kwa ajili ya kuwaletea maendeleo yao ya kiuchumi.
“Sasa wakati umefika Kwa Waislamu ikiwemo na taasisi zake kuwatumia wataalamu waliopo hapa nchini, kwa ajili ya kuweza kujiletea maendeleo ikiwemo kukamatia fursa za kiuchumi zilizopo,”amesema Mufti Zubeir.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Maulid Surumbu amesema kuwa serikali mkoani Tanga ipo tayari kutoa ushirikiano kwa taasisi zote zadini katika shughuli za kimaendeleo.
Nae Mratibu wa ujenzi wa mradi wa hospitali, Ayub Kidege amesema kuwa mradi huo unatekelezwa kutokana na michango mbalimbali ya waislamu.