Waja na Dua ya Kuwaombea Viongozi Wakuu wa nchi
DAR ES SALAAM: Taasisi ya Beach menijimenti unit (BMU) ikiongozwa na Mratibu wa Dua Maalumu ya kuombea Taifa na Viongozi wa Madrasa Hidaya Islamic Centre wameandaa kongamano la kuwaombea Rais Dk Samia Suluhu Hassan na Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi litakalofanyika viwanja vya mnadani kigamboni Oktoba 7,2023.
Hayo ameyasema Omary Kombe Mratibu wa Dua hiyo leo Oktoba 3,2023 Jijini Dar es salaam wakati wakizungumza na waandishi wa habariĀ na amesema Dua hiyo ina dhamira ya kudumisha amani na upendo katika jamiiĀ na kuwaombea viongozi hao waendelee kuliongoza taifa amani na Upendo.
Aidha ameongezea kwa kusema Taifa linakumbwa na janga la ukatili wa kijinsia na ukosefu wa maadili hivyo ameiomba jamii kuacha matendo ya ukatili.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hidaya Islamic Center Twahili Mtoro amesema Dua hiyo ni ya pamoja haina ubaguzi wa dini wala rangi na ametoa wito kwa walimu wa Madrasa kuiombea nchi na viongozi wake.
Dua hiyo inatarajia kushirikisha vituo vya kulelea watoto yatima,viongozi wa dini, vyama vya siasa na jamii kwa kwa ujumla