WATAALAMU kutoka vyuo vikuu viwili vya vya Taasisi ya Afrika ya Sayansi, Teknolojia ya Nelson Mandela(NM-AIST) na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wamekutana na watunga sera kutoka wizara mbalimbali kwaajili ya kuangalia jinsi gani mradi wa maabara ya Akili Bandia kwa Maendeleo ya Afrika utakavyosaidia changamoto za kijamii katika magonjwa na mifugo
Akifungua majadiliano ya wataalam hao na watunga sera katika Chuo hicho,Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandela ,Elimu, Utafiti na Ubunifu, Profesa Anthony Mshandeti amesema wataalamu hao wamekutana kwa pamoja ili kubaini jinsi gani kompyuta inavyoweza kufanya kazi katika tafiti,bunifu na kilimo ikiwemo kubaini aina za magonjwa kwa binadamu na mifugo.
Amesema mradi wa akili bandia ni mradi mkubwa wa kisayansi itakayotumika kwaaajili ya kubaini magonjwa mbalimbali ya wanyama na binadamu ili kuyadhibiti lakini pia watunga sera nao waujue ili waweze kuuingiza katika miongozo mbalimbali itakayosaidia hata wizara mbalimbali kubaini magonjwa yanayoibuka kwa haraka kwakutumia kompyuta
Naye Mtafiti Mkuu wa mradi huo wa akili bandia (AI4D Research Lab Project) Dk,Ally Nyamawe amesema mradi huo ni wakisayansi unaosaidia watafiti kubaini kwa haraka aina mbalimbali za magonjwa kwa binadamu na wanyama na kudhibiti ni wa miaka mitatu na wenye gharama ya sh,bilioni 1.8
Amesisitiza teknolojia hiyo ili iweze kushika kasi zaidi ni vema watunga sera na watoa maamuzi kuelewa mradi
huo katika tafiti,bunifu na mafunzo ili kuwezesha kubaini changamoto za sekta kilimo, uchumi wa kidigitali,afya ikiwemo kubaini wabunifu katika kutatua matatizo tofauti katika jamii hususan kilimo, afya na mifugo
[10:35, 30/03/2023] @Mrtarafa: picha?