Waje tumalizane!

SINGIDA; Ligi Kuu Tanzania Bara itaendelea leo michezo minne ikipigwa katika viwanja tofauti, mkoani Singida Ihefu (Singida Black Stars) watawaalika Simba katika Uwanja wa CCM Liti.
Simba wameupania mchezo huo wakitaka kurejesha tabasamu ndani ya timu yao baada ya kipindi cha mpito cha ukame wa ushindi kikosini hapo, wakati Simba wakipiga hesabu hizo kocha wa Ihefu Mecky Mexime ametamba kutoa burudani ya aina yake kwenye mchezo huo kutokana na ubora wa timu zote mbili.
Mchezo mwingine wa ligi hiyo namba sita kwa ubora Afrika, Saa nane mchana matajiri wa dhahabu Geita Gold watakipiga na wakata miwa Mtibwa Sugar huku Tabora United ikimkaribisha JKT Tanzania.
Mchezo wa mwisho kwa leo Kagera Sugar wakiwa dimba la Kaitaba watakumbana na Dodoma Jiji FC.
 

Habari Zifananazo

Back to top button