Wajifungia kujadili usawa wa kijinsia

DAR-ES-SALAAM: Katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani wadau mbalimbali ikiwemo Hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam, Taasisi ya Huduma za Afya za Kiwango cha Juu na wadau wengine wamekutana Kutambua mabadiliko ya tabianchi kama tishio kubwa la afya ya mwanamke ulimwenguni kama Ilivyotambuliwa na Shirika la Afya Ulimwenguni WHO.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa The Choice, Mratibu wa Kitaifa wa Muungano wa Tanzania wa Jinsia na Mabadiliko ya Tabianchi (GCCTC) Maria Matui amesema wananchi wengi bado hawafahamu kuhusu madhara ya moja kwa moja ya mabadiliko ya tabianchi hivyo miradi kama hii ni muhimu kwa ukombozi wao.

“Si zaidi ya asilimia 24 ya wananchi wanaoishi vijijini wanafahamu madhara ya mabadiliko ya tabianchi au tabia nchi kwa ujumla wake lakini hii haimaanishi kwamba ufahamu wao si sawa na ule ambao labda sayansi inatambua au maandiko mbalimbali ya kitafiti yanachambua”.

Advertisement

Kwa upande wake kiongozi wa mradi wa huo wa Choice Profesa Ahmed Josabani amesema malengo makubwa ya mradi huo ni kutekeleza vipengele vitatu vya dira ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja na afya, usawa wa kijinsia na mazingira huku akitaja Vita ya Urusi na Ukraine na Uviko-19 kama changamoto zilizokwamisha kutekelezwa mapema kwa mradi huo.