Wajivunia kutoa kipaumbele kwa Watanzania

KAMPUNI  ya Dough Works, imesema inajivunia kutekeleza kwa vitendo kauli ya serikali kuhusu kutoa kipaumbele kwa Watanzania katika masuala mbalimbali ikiwemo ajira.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mgahawa mpya wa BAO Cafe, Masaki Dar es Salaam Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Vickram Desai, ameeleza mpaka sasa kampuni yake imetoa ajira zaidi ya 2000 kwa vijana wa mikoa mbalimbali ya Tanzania na kulipa kodi kwa wakati.

“Nafurahi kuona leo tumekutana kuzindua mgahawa wetu mpya wa BAO Café hapa Masaki, ni wa tano katika migahawa ya kisasa Tanzania, lengo letu ni kutoa huduma ya haraka ya chakula kwa wakazi wa Dar es Salaam kutokana na foleni za barabarani, lakini pia uwepo wa  mgahawa huu umeongeza idadi ya watumishi kwenye kampuni yetu,” amesema Desai.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Vivo Energy Tanzania, ambao wanashirikiana na Dough Works, Stan Mittelman, amesema amefurahishwa na muunganiko wao huo na lengo ni kuwasogezea karibu wateja huduma mbalimbali ikiwemo chakula na vilainishi vya magari na mafuta.

“Mahitaji ya bidhaa za nishati yanaongezeka mwaka hadi mwaka nchini Tanzania na Vivo Energy, inapanua shughuli zake na kutoa ajira nyingi kwa vijana wa Kitanzania,” amesema Mittelman.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x