Wajivunia mafanikio usalama wa anga
DAR ES SALAAM: TANZANIA imeadhimisha Siku ya Usafiri wa Anga Kimataifa kwa kufanya maandamano ya kujivunia usalama uliopo katika anga la nchi, hali inayofanya usafiri huo kuwa salama zaidi nchini.
“Lengo hasa la siku hii ni kukumbushana majukumu yetu ya kuhakikisha kwamba tunasimamia shughuli za usafiri wa anga na kuhakikisha kwamba anga letu na hata anga jirani linakuwa salama,” amesema Mbilinyi.
Naye Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege, Flora Mwanshinga amesema kwa sasa wanatekeleza mradi mpya na mkubwa wa kubadilisha mitambo ya sauti ya analojia na kugeukia mitambo ya kidigitali itakayowasaidia marubani na waongoza ndege.
“Kusimika ile mitambo hasa itaanza mwezi Januari, tunategemea ndani ya miezi mitano, mradi utakuwa umekamilika,” amesema Mwanshinga.
Sherehe hizo hufanyika Desemba 07 ya kila mwaka, iliyoasisiwa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO), Tanzania ni nchi mwanachama.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni ‘Ubunifu endelevu kwa Maendeleo ya Usafiri wa Anga Duniani’.