Wajivunia mwitikio wa sensa Kongwa

ZIKIWA zimebaki siku tatu kabla ya kumalizika kwa Sensa ya Watu na Makazi, Diwani wa Kata ya Chamkoroma, Wilaya ya Kongwa, Simon Binde na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani Dodoma, Pili Mbaga wameendelea kuhamasisha wananchi wa wilaya hiyo kushiriki sensa kikamilifu.

Sensa ya watu na makazi ilianza rasmi Agosti 23, 2022 na itamalizika Agosti 29.

Akizungumza kwenye mkutano wa hamasa diwani wa Chamkoroma, Simon Binde, amesema wameendelea kutoa elimu kupitia mikutano mbalimbali ya hadhara na wananchi wameonesha mwitikio mkubwa kushiriki.

“Mwitikio ni mkubwa kwa kweli wananchi wetu wanaendelea kupata elimu ya umuhimu wa sensa na wamekuwa mabalozi wazuri miongoni mwao, wanaendelea kuhamasishana kuweka taarifa muhimu, ili kurahisisha utoaji wa taarifa kwa karani wa sensa wanaoendelea kupita katika maeneo mbali mbali,” amesema.

Kwa upande wa Katibu wa CCM, Pili Mbaga amesema hamasa ni kubwa akiwataka, wananchi kutunza kumbukumbu za familia zao, ili kuwasaidia makarani wa sensa kupata takwimu sahihi.

Habari Zifananazo

Back to top button