DAR ES SALAAM: ZAIDI ya wajasiriamali 500 wamenufaika na fursa za kibiashara kwa kuuza bidhaa mbalimbali pamoja na kutengeneza mtandao kupitia wadau kutoka Kanda ya Afrika Mashariki na Kati walioshiriki Tamasha la Serengeti Lite jana Fukwe za Coco, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika tamasha hilo, Meneja Mawasiliano na Uendelevu Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Rispa Hatibu, amesema kuwa licha tamasha kutoa burudani kupitia kwa wasanii kutoka ndani na nje ya nchi, pia limekusudia kuinua vipato vya wajasiriamali wadogo katika kuuza bidhaa pamoja na kujitangaza.
Nao baadhi ya wajasiriamali walioshiriki katika tamasha hilo wamesema kuwa ni fursa ya kipekee ambayo wameipata ya kujitangaza, huku wakitoa wito kwa wadau wa maendeleo kuendelea kuwashirikisha kushiriki katika matamasha mengine kwa ajili kufungua kutafuta fursa za kibiashara.
Comments are closed.