Wakabidhiwa vyerehani Katavi

HALMASHAURI ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, imekabidhi vyerehani vinne  kwa kikundi cha vijana cha Umoja wa Mafundi Nguo kutoka mfuko wa maendeleo ya vijana chini ya ofisi ya Waziri Mkuu.

Akikabidhi vyerehani hivyo, Meya wa Manispaa ya Mpanda, Haidary Sumry, amewataka wanufaika wa vyerehani hivyo kuvitunza na kuiomba idara ya maendeleo ya jamii ya halmashauri hiyo kuweka utaratibu na ufuatiliaji, ili kujua kama vitendea kazi hivyo vinatumika katika malengo yaliyokusudiwa.

Mwakilishi wa kikundi cha vijana wa Umoja wa Mafundi Nguo, Joseph Mhango, ameishukuru serikali kwa ruzuku hiyo ya vitendea kazi na kuahidi kuwa watazitumia vyema vyerehani hivyo, ili kujiongezea kipato.

Kwa upande wake Mkurungenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Sophia Kumbuli, amewataka vijana kujiunga katika vikundi ili kunufaika na ruzuku hiyo, ikiwemo mkopo usio na riba kutoka halmashauri.

Habari Zifananazo

Back to top button