Wakaguzi jeshi la polisi watakiwa kusimamia haki

MWANZA:Askari Wakaguzi wa Jeshi la Polisi 112 waliohitimu mafunzo ya utayari awamu ya pili yaliyofanyika kwa miezi miwili Mkoani Mwanza, wametakiwa kwenda kutenda haki wakati wanaitumikia jamii ili kudhibiti vitendo vya uhalifu na kuleta usalama.

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza  Wilbroad Mutafungwa wakati akifunga mafunzo ya utayari kwa awamu ya pili kwa Wakaguzi hao katika uwanja wa Polisi Mabatini Jijini Mwanza, Kamanda Mutafungwa amewataka Wakaguzi hao kusimamia haki kwa kuzingatia nidhamu na uadilifu katika jamii wanayoihudumia ili kuhakikisha usalama unaongezeka.

“Kasimamieni watu wapate dhamana kwenye vituo, kapigeni marufuku vitendo vya rushwa na vitendo vyote vibaya ndani ya Jeshi la Polisi na nendeni mkaanzishe vikundi vya ulinzi shirikishi kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa kwa kuwapa elimu ya namna ya kuzuia uhalifu”Amesema

Akieleza lengo la mafunzo hayo kamanda Mutafungwa amesema ni kuwaimarisha wakaguzi hao na kuwaandaa ili wafanye kazi kwa ufanisi zaidi.

“Lengo la mafunzo haya ni kuwaimarisha katika utendaji kazi wa kila siku, tunatarajia viongozi waandamizi wa Jeshi la Polisi watoke miongoni mwenu, ndio maana tuliwasimamia kwa ukaribu na kuhakikisha mafunzo yanafanyika kwa ufanisi”amesisitiza¬† Mutafungwa

Akitoa taarifa ya mwenendo wa mafunzo hayo, Afisa Opereseheni Mkoa wa Mwanza ACP Aloyce Nyantora amesema mafunzo hayo yatakuwa na tija kubwa katika kuimarisha usalama wa wananchi wa Mkoa wa Mwanza kwani mabadiliko mazuri ya kiutendaji yameanza kuonekana.

Nao wahitimu waliopata mafunzo hayo ya miezi miwili kupitia risala yao iliyosomwa na Mkaguzi Ponsian Kalinjuma wameeleza namna mafunzo hayo yatakavyowasaidia kwani wameongeza mbinu mpya ya kupamba na kuzuia uhalifu.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button