Wakandarasi watakiwa kuwa wazalendo

Wakandarasi watakiwa kuwa wazalendo

WAKANDARASI wanaosimamia miradi ya maji mkoani Tanga, kuwa waadilifu na wenye uzalendo kwa kuhakikisha miradi waliyopewa inakamilika kwa wakati na viwango bora.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omari Mgumba wakati wa hafla ya utiaji saini wa mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji na wakandarasi tisa, ambao watahusika katika ujenzi wa miradi yenye thamani ya Sh Bil 10 kwenye wilaya zilizopo mkoani humo.

Advertisement

Amesema kuwa fedha hizo ni nyingi, hivyo matumaini ya serikali na wananchi ni miradi hiyo kukamilika kwa wakati na kumaliza changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji .

“Niwaombe licha ya kuwa waadilifu mkahakikishe mnatoa ajira zile ambazo hazihitaji ujuzi kwa vijana walioko kwenye maeneo ya miradi, ili nao wanufaike na fursa ya fedha hizo,”amesema RC Mgumba.

Naye Meneja wa RUWASA mkoa wa Tanga, Upendo Lugongo amesema kuwa mikataba hiyo imehusisha wakandarasi nane na mkandarasi mshauri mmoja, ambapo zaidi ya wananchi 200,000 wataweza kunufaika na upatikanaji wa huduma ya maji pindi miradi itakapokamilika.

Mkuu wa wilaya Kilindi, Abel Busalama amesema kuwa wilaya yake imepata mradi mmoja wenye thamani ya Sh Bil 6.9, ambapo utakapokamilika kiwango cha huduma kitaongezeka kutoka asilimia 43 hadi 79.8%.

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *