Wakazi 4115 kunufaika na mradi wa maji Newala

ZAIDI ya wakazi 4115 kutoka katika vijiji mbalimbali Halmashauri ya Wilaya ya Newala mkoani Mtwara watanufaika na Mradi wa Maji wa Mchome na Makukwe unaogharimu zaidi ya Sh milioni 331.

Akizungumzia namna ambavyo mradi huo utavyowanufaisha wananchi wilayani humo baada ya mbio za Mwenge wa Uhuru kutembelea na kuweka Jiwe la Msingi katika mradi huo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mandala, Ismail Lukanda amesema zaidi ya wakazi 300 kwenye Kijiji chake watanufaika na huduma hiyo.

Hata hivyo ujio wa mradi utaondoa changamoto ya maji iliyokuwa ikiwakabili wakazi wa kijijini hapo kwani walikuwa wakipata huduma ya maji katika mto Kitangari uliyopo wilayani humo.

Baadhi ya wakazi wa Kijiji hicho akiwemo, Nurdin Rajabu ameishukuru serikali kuwaletea mradi kwani ilikuwa kiu ya mda mrefu kwa wakazi hao na sasa wanajionea maendeleo hayo yanayofanywa na serikali yao ya awamu ya sita.

Fatuma Abeid mkazi wa Kijiji hicho “Ujio wa mradi huu ni faida kubwa sana kwetu sisi wananchi kwasababu zamani kabla ya mradi tulikuwa tunanunua ndoo moja ya maji kwa Sh 500 lakini sasa hivi tunapata huduma kwa urahisi tunanunua Sh. 50 ndoo moja”,

Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWAS) (RUWASA) wilayani humo Mhandisi, Nsajigwa Sadik amesema mradi ulianza kutekelezwa Januari 2022 na unatarajiwa kukamilika Mei 2023 ambapo mpaka sasa umefikia asilimia 100 chini ya mkandarasi ULM Investment Company Limited.

Akizungumza kwa niaba ya Wakandarasi wazawa, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo inayotekeleza mradi huo wa maji ya ULM Investment Company Limited Mhandisdi , Mwanahamisi Ngalemwa ameishukuru Serikali kwa kuwawezesha wakandarasi hao wazawa kwa kuwapatia miradi,kazi wakandarasi hasa Wanawake katika miradi hiyo ya maji (RUWASA) kwani wana uwezo na uthubu wa hali ya juu.

Amesema kwa nafasi yao kama wakandarasi wanawake watahakikisha wanatekeleza kikamilifu miradi hiyo kupitia uwezeshaji mkubwa unaofanywa na Serikali kupitia Wizara husika ili kuleta ufanisi kwenye sekta hiyo.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim ameridhia mradi huo na kuweka jiwe la msingi huku akisisitiza suala la upandaji wa miti kwenye chanzo ili kukifanya chanzo hicho kiwe imara.

Aidha mradi huo unaenda kunufaisha wakazi kutoka Vijiji mbalimbali Wilayani humo ikiwemo Mandala, Namkonda, Mpotola, Mnali na Mkupete.

Habari Zifananazo

Back to top button