Wakazi Kilimawe kunufaika na mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria

WAKAZI zaidi ya 2000 kutoka kijiji cha Kilimawe kata ya Mwantini Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wameanza kunufaika na mradi wa majisafi na salama kutoka Ziwa Victoria uliotekelezwa kwa zaidi ya Sh milioni 159.

Meneja wa Wakala wa Majisafi na Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Shinyanga Mhandisi Emaeli Nkopi aliyasema hayo jana mbele ya viongozi wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT ) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga ambapo alieleza mradi huo umetekelezwa kwa siku 170 na kukamilika.

“Wananchi sasa wameanza kunufaika na mradi wa maji nakuwaondolea adha ya kununua maji au kuyafuata umbali mrefu kwani ulianza rasmi tarehe 6,Juni,2023 na 30,Novemba,2023 umekamilka na umesanifiwa kuhudumia wanachi 2,262.” alisema mhandisi Nkopi.

Nkopi alisema gharama ya mradi fedha ilitengwa zaidi ya Sh milioni 333 na fedha iliyotumika ni zaidi ya Sh milioni 159 na kiasi kilichobaki ni zaidi ya Sh milioni 173 ambacho kitaelekezwa kwenye shughuli zingine ili kuondoa changamoto.

Mhandisi Nkopi aliwataka wananchi wajitokeze kuvuta maji majumbani kwa kuwaona jumuiya za watumia maji (CBWSO) ambao watawapa utaratibu wa kuijiunga na fedha zinalipwa kwa njia ya mfumo.

Mbunge viti maalum Santiel Kirumba ambaye aliongozana na viongozi wa UWT mkoani Shinyanga alisema kazi imefanywa vizuri na Ruwasa ambapo mradi umekamilika kwa kutekelezwa siku 170 na fedha zimebaki hivyo serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia ndiyo inavyotaka kazi iendelee. .

“ Kitu ambacho kimemfurahisha zaidi ni fedha kubaki katika mradi huu na nimewaomba wananchi maji hayo ni hazina wayatumie vizuri kwa kutunza miundombinu kwani Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa maono yake kipaumbele ni Elimu,afya na maji.”alisema mbunge Kirumba.

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Shinyanga Grace Samweli alisema wanasimamia ilani ya (CCM) kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama hivyo wanaume nao wanatakiwa kupongeza juhudi hizi ambazo zilikuwa zikiwafanya wanawake kutafuta maji nyakati za usiku nakuacha kufanya shughuli za kijamii.

Katibu wa UWT mkoa wa Shinyanga Asha Kitandala alisema amefurahi kuona utekelezaji unaenda vizuri Zahanati imepata maji kama zipo changamoto ni ndogondogo zitaenda zikitatuliwa ila wanaipongeza Ruwasa kwa juhudi wanazozifanya kwa miradi ya maji.

Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho waliohudhuria mkutano akiwemo Nkohoni Seseko na Jackson Shija waliuliza namna ya taasisi zitakavyolipia ankara za maji na wao kupata maji majumbani ikiwa walifurahi kwani ndoo moja walikuwa wakinunua sh 500 hadi 1000.

Habari Zifananazo

11 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button