Sh milioni 120 kujenga uzio kituo cha afya Bugarama

MGODI wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu uliopo Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga umetoa Sh milioni 120 kwaajili ya ujenzi wa uzio kwenye kituo cha afya Bugarama kinachohudumia zaidi ya wakazi 48,000 .

Mganga mfawidhi wa kituo hicho, DK Silasi Kayanda aliyasema hayo juzi baada ya Kaimu Ofisa Mahusiano na Mazingira kutoka mgodi huo akiwa na waandishi wa habari kutembelea kituo hicho ambapo ameeleza kilianzishwa kuwa Zahanati kukiwa na jengo la Wagonjwa wa nje pekee mwaka 2014.

Advertisement

Dk Kayanda alisema mgodi huo kupitia Fedha za Huduma kwa Jamii (CSR) umekipandisha hadhi kituo hicho mwaka 2016 na huduma zote zinatolewa ambapo wamefanikiwa kupunguza vifo vya watoto wachanga na wajawazito.

“Wamejenga majengo yakutolewa huduma Kama vile Mionzi,Upasuaji,kituo cha watoto njiti,Wodi ya Wajawazito na wanaojifungua,Wodi ya watoto na jengo la kuhifadhia maiti kipindi huduma hizi hazikuwepo watu walilazimika kusafiri umbali wa kilomita 73 kufuata huduma Kahama mjini.”alisema.

Dk Kayanda alisema katika huduma ya mama na mtoto wamepunguza vifo vitokanavyo na uhitaji wa upasuaji kwa siku kina mama 20 hadi 30 wanafanyiwa Upasuaji,wajawazito wanaojifungua kwa siku ni 50 na kliniki ya watoto kwa siku ni 60 hadi 70 wanahudhuria.

Kaimu Meneja Mahusiano na Mazingira kutoka mgodi huo, Zuwena Senkondo alisema kuna miradi 50 ambayo wanatekeleza ambapo kituo hiki wametoa fedha za huduma kwa jamii kwa lengo la kupunguza changamoto ili watu waweze kupata huduma zote karibu.

“Mgodi umetoa Sh millioni 120 kwaajili ya ujenzi wa uzio tuliona hiyo ni kero kubwa iliyo bakia sasa tunakwenda kuimaliza ili Wagonjwa wawe katika hali ya Usalama wakati wa kupata huduma.

“alisema Senkondo.

Diwani wa kata ya Bugarama Prisca Musoma alisema mgodi umekuwa ukitoa fedha za CSR kwenye kata hiyo na wamekamilisha Zahanati tatu zinafanya kazi na kituo Cha afya Bugarama kimeongezewa majengo ikiwemo jengo la mama na mtoto na tayari sh Millioni 120 za ujenzi wa uzio zimetolewa.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Bugarama Jesca Martin na Shimba Gabriel walisema uzio unahitajika kwani kuna malalamiko yalitokea siku za nyuma kutoka kwa wauguzi ndugu wa wagonjwa kuingia bila utaratibu wodini kutokana na kukosa Uzio.

Aidha Halmashauri ya Msalala imekuwa ikipokea Sh bilioni 2 kila mwaka kwaajili ya huduma ya jamii (CSR ) kutoka kwenye mgodi wa dhahabu Bulyanhulu na tayari zahanati 18 zimekarabatiwa kwenye vijiji 12 vinavyozunguka mgodi huo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *