“Wakazi wa Mwanza wachangamkie fursa REA”

WAKAZI wa Mkoa wa Mwanza wametakiwa kutumia fursa ya kuunganishiwa umeme na Wakala wa Nishati vijijini (REA) kabla ya kukamilika kwa miradi mbalimbali inayotekelezwa mkoani humo.

Rai hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati vijijini (REA) Janet Mbene wakati wa ziara ya bodi hiyo ilipotembelea miradi yake Wilaya ya Magu na Ilemela.

Advertisement

Amesema uhitaji wa umeme kwa wananchi wengi bado ni mkubwa sana. Amesema gharama za kuunganishiwa umeme wa REA ni Sh 27,000.

Mbene amewapongeza wakazi wa mtaa wa Nyamadoke wilayani Ilemela kwa ushirikiano waliotoa kwa wakandarasi wakati wa kuunganishiwa umeme.

Ameahidi wakazi wa kijiji cha Busekwa Wilaya ya Magu watawekewa umeme wakati wa mradi wa ujazilizi. Amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutoa fedha kwa ajili ya kuunganisha umeme kwa wananchi.

Ameahidi kuwa kila kijiji kitawekewa umeme mpaka Disemba 2023. Ameahidi REA itaweka umeme katika shule ya msingi Chief Hangaya iliopo katika Wilaya ya Magu.

Msimamizi wa Miradi ya REA Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Ernest Makale amesema tayari vijiji 544 kwa mkoa wa Mwanza vimeshawekewa umeme.

Amesema kwa wilaya ya Ilemela tayari wakazi 532 wamewekewa umeme kupitia mradi wa Peri urban. Amesema kwa Magu tayari vijiji vyote 51 vimewekewa umeme.

9 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *