Wakenya mbaroni wizi  kwenye magari

TANGA; Jeshi la polisi mkoani Tanga limekamata raia wawili kutoka nchini jirani ya Kenya wakituhumiwa kufanya matukio ya wizi kwenye magari.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa Tanga, Almachius Mchunguzi amewataja watuhumiwa kuwa ni Idrisa Kassim (24) na Samweli Mwenda, ambao walikamatwa Septemba 12 mwaka huu, Barabara ya 13 jijini Tanga.

Amesema watuhumiwa hao walikamatwa vitu mbalimbali vya wizi ikiwemo rimoti ambazo zinatumika kufungua milango ya  magari pamoja na mageti.

Advertisement

 

7 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *