Wakili Mkono afariki dunia

WAKILI maarufu nchini na aliyewahi kuwa Mbunge wa Musoma Vijijini na Butiama, Nimrod Mkono (80) amefariki dunia jijini Florida nchini Marekani alikokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa za aliyejitambulisha kuwa ni mdogo wa marehemu, Zadock Mkono na mtoto wa marehemu, Leah Mkono wamethibitisha kuwa wakili huyo ameaga dunia.

“Ni kweli, Mheshimiwa Nimrod Mkono hatunaye tena, nimezungumza kwa simu na mke wake pamoja na binti yake wanaoishi Ulaya ambako mauti yamemkutia, wamenithibitishia hilo,” alisema Zadock jana usiku.

Zadock alieleza kuwa mwanasiasa huyo aliyekuwa mbunge wa Musoma Vijijini kuanzia mwaka 2000 hadi 2015 na baadaye Jimbo la Butiama kuanzia mwaka 2015 hadi 2020 atazikwa hapa nchini na taratibu zikikamilka familia itatoa taarifa.

Mkono alizaliwa Agosti 18, 1943 na alikuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mkono aliyefanya kazi za uwakili Tanzania Bara na Zanzibar ameacha mjane na watoto wanne.

*Imeandikwa na Editha Majura (Singida) na Fransisca Emmanuel (Dar es Salaam).

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x