Wakili wa Odinga adai IEBC haiwezi kuaminiwa

WAKILI mkuu  James Orengo wa mgombea urais wa Azimio la Umoja nchini Kenya Raila Odinga, ameiambia Mahakama ya Juu kwamba Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) haiwezi kuaminiwa kufanya uchaguzi wa kuaminika nchini humo.

“Tuna tume ambayo imegawanyika katikati kabisa, tunazungumzia tume ambayo haifanyi kazi yake na haiwezi kufanya uchaguzi. Mnara wa Babeli umeangushwa,” Orengo alisema.

Orengo alisema kuwa taasisi zote huru zinahitajika kuheshimu mamlaka ya watu, na mamlaka lazima yatekelezwe kwa mujibu wa Katiba lakini IEBC imeshindwa katika suala hili jinsi ilivyoendesha uchaguzi wa urais.

Makamishna wanne wa IEBC walijitenga na matokeo yaliyotangazwa na mwenyekiti Wafula Chebukati wakisema kwamba hawakuweza kuthibitisha nambari hizo kutokana na “kutokuwa na uwazi” wa mchakato huo kama ulivyoendeshwa na bosi wao.

Hata hivyo, Chebukati amedai kuwa wanne hao walitaka adhibiti matokeo ili kutangaza kuwa hakuna mgombeaji urais aliyeshinda na kusukuma nchi katika uchaguzi mpya kati ya wagombeaji wawili wakuu.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x