Wakimbizi 1,500 kutoka Libya kupokelewa Italia

SERIKALI ya Italia itawapokea wakimbizi na wanaotafuta hifadhi 1,500 kutoka Libya katika kipindi cha miaka mitatu ijayo, kufuatia makubaliano na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi.

Mpango uliopo ni upanuzi wa mipango ya awali ya makazi mapya, ambapo Italia iliwahamisha wakimbizi 1,300 na watafuta hifadhi kutoka Libya.

Miongoni mwa wale ambao tayari wamepewa makazi mapya katika mipango ya awali ni pamoja na wakimbizi na wanaotafuta hifadhi ambao walikuwa wamehamia Libya kutoka nchi nyingine za Afrika.

UNHCR ilisema inakaribisha mpango wa kuwahamisha wakimbizi kwa vile unatoa njia muhimu ya maisha kwa wakimbizi na wanaotafuta hifadhi wanaokabiliwa na hatari kubwa ya ulinzi.

Habari Zifananazo

Back to top button