Kocha wa Brazil, Adenor Leonardo Bacch ‘Tite’ amethibitisha kuwa nyota Neymar Jr amepona majeraha na atakuwepo kwenye mchezo wao raundi ya 16 bora dhidi ya Korea Kusini kesho.
Nyota huyo wa Paris Saint-Germain alipata jeraha la kifundo cha mguu wakati wa mechi ya kwanza ya makundi dhidi Serbia yaliyofanya kukosa michezo miwili ya hatua hiyo. kati ya Uswis na Cameroon.
Kuhusu Neymar, “atafanya mazoezi leo mchana na ikiwa yuko sawa, atacheza kesho. Sishiriki habari yoyote ambayo si ya kweli. Jibu langu ni atafanya mazoezi mchana huu, kila kitu kikiendelea vizuri atacheza.” amesema Tite.
Kurejea kwa Neymar kunaleta matumaini mapya kwenye kikosi hicho, hasa baada ya kuumia mshambuliaji wa Arsenal Gabriel Jesus kutokana na jeraha la goti alilopata dhidi ya Cameroon na Alex Telles aliyeumia pia