Wakubali kuhamia Msomera

MSEMAJI wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema jumla ya kaya 30 zenye watu 224 na mifugo 339 wamekubali kuhama kwa hiari kutoka Ngorongoro kwenda Msomera.

Akitoa taarifa za Serikali kwa wanahabari mapema leo jijini Dar es Salaam, Matinyi amesema wakiwa wameingia katika awamu ya pili ya kuwahamisha wananchi kutoka eneo lililotengwa hadi Msomera tayari wananchi wapatao 500 wameshaandikishwa ambapo tayari wameshafanya tathmini ya mali za 400 kwa ajili ya malipo.

“Ndani ya mwezi huu wa kwanza kaya nyingi zitahama kwa sababu zipo 350 ambazo tayari zimefanikisha.

” Amesema Matinyi.

Ameongeza kuwa Serikali ina mpango wa kujenga nyumba 5,000 ambazo zitakuwa na uwezo wa kubeba wananchi 115,000.

Hata hivyo amesema kwa waliochagua kuhamia maeneo mengine waliyochagua ni kaya 25 zenye watu 172 na mifugo 213 na zote kwa pamoja zilizohamia maeneo mengine tofauti na Msomera ni kaya 52 zenye watu 292 na mifugo 982.

Matinyi alisisitiza kuwa zoezi hilo lilikuwa la hiari na serikali iliamua kuwahamisha wananchi hao kwa ajili ya kujiletea maendeleo yao na ya eneo la hifadhi.

Habari Zifananazo

Back to top button