Wakulima 15 Nigeria wauawa

WAKULIMA 15 wa zao la mpunga wameuawa na wengine kutekwa nyara katika jimbo la Borno Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, inadhaniwa kundi la wanamgambo la Boko Haram limehusika huku vijiji vitatu vikishambuliwa, kiongozi wa wakulima eneo hilo ameeleza.

Shambulio hilo lilitokea katika vijiji vya Koshebe, Karkut, na Bulabulin katika eneo la Serikali ya Mtaa ya Mafa katika jimbo hilo, takriban kilomita 15 kutoka mji mkuu wa Maiduguri, Mohammed Haruna, katibu wa Chama cha Wakulima wa Mpunga cha Zabarmari, mtandao wa Reuters umeripoti.

Haruna alisema kundi hilo lilivamia wakiwa na pikipiki na kuwashambulia wakulima waliokuwa wakivuna mazao kwenye mashamba ya mpunga.

“Hawakutumia bunduki kuwaua, badala yake walitumia mikato na visu kuwaua, huku wengine wakikatwa vichwa.” alisema Haruna.

Habari Zifananazo

Back to top button