WAKULIMA 956,920 wamesajiliwa kwa ajili ya kupata mbolea ya ruzuku, ambapo jumla ya tani 60, 882 za mbolea zimenunuliwa na wakulima katika Mikoa ya Arusha, Iringa, Mbeya, Morogoro, Njombe, Rukwa, Ruvuma na Songwe.
Hayo yamesemwa leo Septemba 23, 2022 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati akiahirisha Mkutano wa Bunge la 12 mjni Dodoma.
Amesema wastani wa matumizi ya mbolea nchini katika kipindi cha mwaka 2019/2020 na 2021/2022 umeendelea kuwa tani 430 ,000 na kwamba hadi kufikia Agosti 31, 2022 upatikanaji wa mbolea umefikia tani 213,403, sawa na asilimia 49.6 ya wastani wa matumizi ya mbolea.
Amesema fedha zilizoidhinishwa na Rais Samia Suhulu Hassan, Sh bilioni 150 wa ajili ya mbolea ya ruzuku, imelenga kuwezesha upatikanaji wa bidhaa hiyo kwa wingi na kwa gharama nafuu.