Wakulima Kusini waeleza walivyojifunza Nanenane

WAKULIMA Kanda ya Kusini katika mikoa ya Lindi, Ruvuma na Mtwara wameeleza namna wanavyonufaika na Maonesho ya Nane nane yaliyofanyika katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.

Wakulima hao wamepata fursa ya kuzungumza na HabariLeo mapema leo Agosti 8, 2023 na kufafanua jinsi walivyonufaika.

 


Ibrahim Hassan mkulima kutoka Kitaya mkoani Mtwara amesema amejifunza masuala mbalimbali ikiwemo uandaaji na utunzaji wa shamba, mavuno pamoja na uhifadhi wa mbegu hivyo amezipongeza taasisi mbalimbali zinazotoa huduma hiyo kwa wakulima na serikali kwa ujumla kwa jitihada za kuboresha sekta hiyo.

Diwani kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Newala mkoani Mtwara, Jamali Jafu ameishauri serikali kuwa kuanzia msimu huu iwakopeshe wakulima hao mbegu bora, mbolea pamoja utoaji wa elimu zaidi juu ya utunzaji wa shamba ili kuleta tija zaidi kwenye uzalishaji.

Amesisitiza kuwa,” Tukopeshwe mbolea na tupatiwe elimu zaidi kuhusu utunzaji wa shamba kwahiyo mimi ninachokiomba kwa serikali suala la mbolea, mbegu bora”.amesema Jafu

Ofisa Kilimo wa Kampuni ya SEED CO nchini, Hassan Rajabu amesema kampuni hiyo mbali na utoaji elimu iko kuhakikisha mkulima anafanya vizuri katika kazi yake wampatia mbegu na mtaalam wa kilimo bila malipo kwa ajili ya kupatiwa huduma hiyo kwa uhakika zaidi na tangu kuanza maonesho hayo mwitikio wa Wakulima ni mkubwa kwasababu wamepokea idadi kubwa ya wakulima waliyokuja kujifunza kwenye kampuni yao.

“Wakulima wengi wamekuja na tumewapatia mafunzo mbalimbali na wakahamasika kununua mbegu zetu kwahiyo tunawashauri wakulima kabla hawajaanza kufikiria nilime nini ahakikishe kwanza anakuwa na mbegu bora na inayomfaa”,

Maonesho hayo ya Kanda ya Kusini yanafungwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas na yalifunguliwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Jumanne Sagini

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button