SINGIDA: RAIS Samia Suluhu Hassan amewataka Wananchi wa Wilaya ya Mkalama kulima kwa juhudi kwani Serikali imetengeneza mazingira mazuri kwa umwagiliaji na kutoa pembejeo.
Kuhusu masoko, kiongozi huyo amesema Serikali hailali katika kuhakikisha wanapata masoko ya mazao yao yanakuwa ni ya uhakika.
Amiri Jeshi Mkuu amesema hayo Oktoba 16, 2023 wakati akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Mkalama, mkoani Singida.
“Kwahiyo niwahakikishieni limeni masoko yapo, kama soko la nje halipo kwa wakati huo serikali itanunua yale mliyozalisha,” Amesema Rais Samia.
Aidha, Rais Samia amewataka wananchi kila mmoja kwa nafasi yake kufanya kazi kwa juhudi ili kupelekea maendeleo yake na taifa kwa ujumla.
Pia, Rais amewataka wananchi hususani wa mabondeni kukaa kwa tahadhari kutokana na matarajio ya uwepo wa mvua kubwa za El-Nino kuanzia mwezi huu.
Comments are closed.