Mtwara watakiwa kulima mazao mchanganyiko

MKUU wa Wilaya ya Mtwara, Hanafi Msabaha amewataka wataalamu wa halmashauri zote wilayani humo kuwahamasisha wakulima kulima zao zaidi ya moja, ili kuwa na uchumi endelevu.

Akizungumza leo mkoani Mtwara katika kikao cha Kamati ya Ushauri cha Wilaya (DCC), Msabaha amewataka wataalamu hao kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi ikiwa pamoja na uhamasishaji wa wakulima kulima mazao mchanganyiko, ili wasitetereke kiuchumi.

“Wataalamu tunao wajibu wa mkubwa kutoa huduma bora kwa wananchi wetu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha tunawahamasisha walime mazao zaidi ya moja ili wasitetereke na hii itasaidia kupata uchumi endelevu,” amesema Msabaha.

Mkuu huyo wa Wilaya amewasisitiza wataalam hao kujenga tabia ya kuwatembelea wananchi katika maeneo yao, ili kufahamu changamoto zinazowakabili na kutafuta njia nzuri ya kuzitatua changamoto hizo.

Msabaha ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye sekta mbalimbali Wilayani humo ikiwemo afya, elimu, Barabara, maji na zingine.

 

Habari Zifananazo

Back to top button