Wakulima korosho waomba usimamizi wa Serikali

WAKULIMA na wadau wa zao la korosho kutoka sekta za Serikali na binafsi wilayani Mtwara, wameiomba Serikali kulisimamia zaidi zao hilo kuwa lenye tija kiuchumi na wakulima kunufaika na pembejeo.

Wakizunguza leo Februari 13, 2023 katika uzinduzi wa kikao cha Baraza la Biashara Wilaya ya Mtwara baadhi ya wakulima wa Kata ya Jengwa Halmashauri ya Mji wa Nanyamba, wamesema ugawaji wa pembejeo uzingatie mahitaji halisi ya mkulima au idadi ya mikorosho ili kuleta tija katika uzalishaji.

‘’Kumekuwa na changamoto ya ugawaji wa pembejeo ya ruzuku iliyotolewa bure na serikali yetu, utaratibu wa ugawaji haukuzingatia mahitaji ya mkulima kujua anahitaji kiasi gani cha dawa kwa hiyo ombi letu ili tuweze kuboresha zao hili liwe lenye tija ugawaji wa dawa uzingatie haki kwa kuangalia mahitaji ya mkulima’’,amesema Issa Abdallah mkulima kutoka katika kata hiyo.

Advertisement

Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, Shadida Ndile ameunga mkono suala hilo kwa kusisitiza suala la pembejeo za korosho, ili kukuza uzalishaji ambao utasaidia kumuinua mkulima kiuchumi kupitia zao hilo.

“Pembejeo ikiwa na tija uzalishaji unaimarika kutokana korosho inayozalishwa inakuwa na ubora mzuri unaostahili na inapouzwa soko linakuwa zuri kwa hiyo mzunguko wa kiuchumi unakuwa kwa wakulima ,wananchi wetu na mkoa kwa ujumla,’’amesema Ndile.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *